Saturday, June 29, 2013

MAMIA NCHINI AFRIKA KUSINI WAJITOKEZA KATIKA MAANDAMANO YA AMANI YA KUPINGA KUJA KWA RAISI OBAMA


 Waandamanaji Nchini Afrika Kusini wakiwa wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa Raisi Obama nchini Humo wakati wa maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika  jana Jioni - Juni 28

 Waandamanaji Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Afrika Kusini Jioni ya jana  Juni 28

 Waandamaji wa Nchini Afrika Kusini wakiwa wanasali mbele ya Ubalozi wa Marekani wakati wa maandamano ya kupinga kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo jana  wakati Raisi Obama alipotua Nchini Humo Kwa Ziara ya Siku 2 ..

Mmoja wa waandamaji nchini Afrika Kusini ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa amebeba moja ya Bango ambalo Linamwita Raisi OBAMA kuwa ni Mpishi wa Ikulu ya Marekani kama linavyosomekana na kuendelea kuelezea kuwa sera za Marekani ni tatizo.Mwandamaji huyu alibeba bango hilo jana  Juni 28 wakati wa maandamo ya amani kuelekea mbele ya Ubalozi wa Marekani NChini humo kwa kupinga Kuja Kwa OBAMA Nchini Mwao.Picha Zote na REUTERS/AFP

Friday, June 28, 2013

CHUO KIKUU HURIA TANZANIA KITAMTUNUKU PhD OBAMA


Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT),kimepanga kumtunuku Rais wa Marekani, Barack Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake kwa jamii husasani kwenye maendeleo ya kukuza uchumi. 
Akizungumza na waandishi wa habari jana,Makamu Mkuu wa chuo hicho,Profesa Tolly Mbwete alisema tuzo hiyo imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa OUT, Dk Asha Rose Migiro.

“Tumeangalia vigezo vyote muhimu ambavyo mtu anastahili kupewa tuzo kama hii na tukaridhika kuwa Rais huyo anastahili kutunukiwa,” alisema Profesa Mbwete.
Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais Obama anakuwa mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na Mwalimu Julias Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Benjamin Mkapa.
Alisema hadi sasa OUT imetoa shahada saba za heshima, ambapo kati ya hizo mbili walitunukiwa mwanataaluma kutoka Marekani, Dk Jane Goodall na Mhadhiri wa Mawasiliano kutoka nchini Uingereza,David Mellor.