Chuo Kikuu Huria Tanzania
(OUT),kimepanga kumtunuku Rais wa Marekani, Barack Obama Shahada ya
Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake kwa jamii husasani kwenye
maendeleo ya kukuza uchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana,Makamu Mkuu wa chuo hicho,Profesa Tolly Mbwete alisema tuzo hiyo
imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa
OUT, Dk Asha Rose Migiro.
“Tumeangalia vigezo vyote muhimu
ambavyo mtu anastahili kupewa tuzo kama hii na tukaridhika kuwa Rais
huyo anastahili kutunukiwa,” alisema Profesa Mbwete.
Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais
Obama anakuwa mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na
Mwalimu Julias Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini,
Nelson Mandela, Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Benjamin Mkapa.
Alisema hadi sasa OUT imetoa shahada
saba za heshima, ambapo kati ya hizo mbili walitunukiwa mwanataaluma
kutoka Marekani, Dk Jane Goodall na Mhadhiri wa Mawasiliano kutoka
nchini Uingereza,David Mellor.
No comments:
Post a Comment