Wednesday, April 17, 2013

PICHA MABALIMBALI ZA MAANDALIZI YA MAZISHI YA BI. KIDUDE

source ;vijimambo
Gari lililokuwa limeubeba mwili wa msanii mkongwe wa muziki wa tarab, marehemu Fatuma Binti Baraka 'Bi. Kidude', likiusafirisha kutoka katika Kijiji cha Kihinani na kuupeleka nyumbani kwake Rahaleo kwa matayarisho ya mazishi yatayofanyika leo mchana katika Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. (Picha zote kwa hisani ya Othman Maulid wa ZanZinews)
Mwili wa marehemu ukishushwa katika gari wakat ukiwasili nyumbani kwake, Rahaleo kwa taratibu za mazishi
Ndugu, Jamaa na marafiki, wakiubeba mwili wa marehemu Bi. Kidude wakati ulipowasili nyumbani kwake, Rahaleo kwa ajili ya matayarisho ya mazishi yatakayofanyika leo  Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Mrajisi wa Baraza la Sanaa la Zanzibar, Khadija Batashi, akizungumza na waandishi wa habari jinsi alivyoupokea msiba wa msanii mkongwe wa muziki wa taraba nchini, Bi Kidude.
Matayarishi ya mazishi ya msanii wa muziki wa tarab, Bi. Kidude yakiendelea nyumbani kwake Rahaleo, mjini Zanzibar.
Mjukuu wa Bi. Kidude Omar Ameir, akiwasiliana na jamaa kwa ajili ya kuwajulisha msiba wa marehemu Bi. Kidude, baada ya mwili wa marehemu huyo, kuwasili nyumba kwake kwa ajilimatayarisho ya mazishi yatakayofanyikaleo mchana baada ya Swala ya Adhuhuri, ambapo atazikwa Kitumba.
Bi. Maryam Hamdani akilakiwa na Bi. Sihaba wakati akiwasili nyumbani kwa marehemu Bi. Kidude Rahaleo, mjini Zanzibar akiwa na majonzi.  
Waandishi wa habari wakizungumza na Mfadhili Mkubwa wa Bi. Kidude, Maryam Hamdan, kuhusiana na marehemu ambaye yeye alikuwa ni mtayarishaji na mratibu wa safari za Bi. Kidude nje ya nchi na katika matamasha mbalimbali aliyokuwa akihudhuria nje ya nchi wakati wa uhai wake.
Meneja wa Sauti ya BUSARA Zanzibar, Stella Steven, akizungumza na waandishi wa habari, mjini Zanzibar kwenye msiba huo, kuhusiana na marehemu Bi. Kidude ambaye alikuwa akidhaminiwa na Sauti za BUSARA katika matamasha mbalimbali yaliokuwa yakiandaliwa na taasisi hiyo  ya sanaa, jinsi walivyopokea kifo chake kwa masikitiko makubwa na kuacha pengo katika tasnia ya muziki wa taarab asilia Zanzibar.  
Picha kwa hisani ya Jestina-George

No comments: