Source;Bongo 5
Wasanii, wadau na wa muziki wa kizazi kipya pamoja na baadhi ya ndugu wa marehemu Albert Mangwea jioni ya jana walikutana kwenye viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuchangishana fedha kusaidia shughuli za mazishi za rapper huyo aliyefariki jijini Johanessburg Afrika Kusini.
Katika mkutano huo, kamati maalum imeundwa na inaongozwa na muongozaji wa video za muziki, Adam Juma, producer wa Bongo Records P-Funk Majani, Profesa Jay, Lady Jaydee, Jay Moe, Nooran na Maze B. Wengini ni pamoja na Mchizi Mox na TID. Pia Noorah amechaguliwa kuwa mweka hazina wa fedha hizo za mchango.
No comments:
Post a Comment